Anza kujifunza leo kwa 100% Vitendo

Jifunze Ujuzi wa Kisasa,
Jenga Kesho Yako

Gundua kozi bora za mtandaoni zinazoongozwa na wataalamu wa sekta. Jifunze coding, kutengeneza mifumo (Apps), UI/UX design na akili mnemba (AI) ili kufungua milango ya mafanikio ya kikazi.

1,500+

Wanafunzi Waliohitimu

80+

Vipindi vya Vitendo

100%

Miradi ya Kazi (Projects)

96%

Kupata Kazi / Kujiajiri

Gundua Kozi zetu za Tech

Chagua ujuzi unaotaka kujifunza leo na upate mafunzo yaliyosheheni miradi ya vitendo.

Mbona Uchague Chuo cha UjuziSafi?

Tunakupa mfumo wa kisasa wa kujifunza unaoondoa nadharia na kuweka mkazo kwenye ujenzi wa miradi halisi ya kibiashara.

Kujifunza kwa Vitendo

Hatusomi tu vitabu! Kila kozi inakuhitaji kutengeneza mifumo, tovuti, au kazi halisi ambazo unaweza kuzionyesha kwa waajiri.

Muda wa Ziada & Unyumbufu

Masomo yetu yanapatikana saa 24/7. Jifunze kwa ratiba yako mwenyewe, ukiwa nyumbani, ofisini, au popote ulipo duniani.

Cheti Kinachotambulika

Ukimaliza masomo yako na kukamilisha miradi yote, utapokea cheti rasmi kitakachokuongezea nafasi ya kupata ajira au wateja.

Shuhuda kutoka kwa Wanafunzi wetu

Tazama jinsi wanafunzi wenzako walivyobadilisha maisha yao na kuingia kwenye soko la tech kupitia mafunzo ya UjuziSafi.

Maswali Yanayoulizwa Sana (FAQs)

Majibu ya haraka kwa maswali unayoweza kuwa nayo kuhusu masomo na mfumo wetu.

Je, nahitaji uzoefu wowote wa coding kuanza masomo?
Hapana! Kozi zetu nyingi zimeandaliwa kuanzia ngazi ya mwanzo kabisa (Beginner Level). Mkufunzi anaanza na misingi, kwa hiyo hata kama hujawahi kuona code maishani mwako, utajifunza kwa urahisi sana.
Mifumo na masomo yanasomwaje? Je kuna muda maalum?
Masomo yote yapo katika mfumo wa video zilizorekodiwa vizuri pamoja na faili za mazoezi (source codes). Unaweza kuingia na kujifunza saa yoyote na siku yoyote inayokufaa kulingana na nafasi yako.
Nitalipaje ada ya kozi?
Tunapokea malipo kupitia mifumo ya simu (M-Pesa, Tigopesa, Airtel Money, HaloPesa) kwa usalama kabisa. Baadhi ya kozi za mwanzo ni za bure kabisa ili uweze kujaribu kabla ya kulipia.

Uko Tayari Kubadilisha Maisha Yako ya Kazi?

Jiunge na maelfu ya wanafunzi wengine wanaojifunza ujuzi wa kisasa na kujenga miradi mikubwa nchini.