VIGEZO NA MASHARTI

Terms & Conditions of Jombay API

Karibu kwenye Mfumo wa API wa Jombay Enterprises. Kwa kutumia API hii na funguo zake za ufikiaji (API Keys), unakubali kufungwa na vigezo na masharti yafuatayo:

1 Usalama na Umiliki wa API Key

Marufuku Kusambaza: API Key uliyopewa ni ya siri na ni kwa ajili ya matumizi ya mfumo wako tu. Ni marufuku kabisa kusambaza, kuuza, kuazima, au kuwapa watu wengine funguo hii kwa namna yoyote ile.
Ulinzi wa Key: Mtumiaji anawajibika kikamilifu kulinda usalama wa API Key yake. Jombay Enterprises haitahusika na uharibifu au matumizi mabaya yanayotokana na uzembe wa mtumiaji kuvujisha key yake.
Uhitaji wa Mfumo: Ikiwa kuna mtu au taasisi nyingine inayohitaji kutumia mfumo huu wa API, hawaruhusiwi kutumia key yako. Wanapaswa kuwasiliana moja kwa moja na Developer wetu mkuu ili kupata leseni na funguo zao wenyewe.

2 Kikomo cha Matumizi (API Calls Limit)

Kikomo cha Awali (Limit): Kila API Key inakuja na kikomo cha mwisho cha kupiga API (Max Limit ya API Calls 500).
Baada ya Kikomo Kwisha: Pindi idadi ya calls 500 inapoisha, mfumo utasimama kuzalisha mikataba kiotomatiki. Mtumiaji atalazimika kulipia upya (Renew) ili kuongeza salio la API calls na kuendelea kutumia mfumo.
Kuangalia Salio: Unaweza kuangalia idadi ya calls ulizotumia na zilizobaki kwa kupiga endpoint yetu ya status wakati wowote.

3 Matumizi Yanayokubalika

API hii inapaswa kutumika tu kwa malengo yaliyokusudiwa (kuzalisha mikataba halali ya Till na Lipa Namba).

Ni marufuku kutumia API hii kufanya majaribio ya kishambulizi (cyber-attacks), kutuma data za uongo kwa makusudi, au kujaribu kuingilia miundombinu ya server yetu.

4 Marekebisho ya Masharti

Jombay Enterprises inahifadhi haki ya kubadilisha au kuboresha vigezo hivi wakati wowote. Watumiaji watafahamishwa mapema kulingana na mabadiliko yatakayojitokeza.
Ilisasishwa mwisho: 26 Nov, 2026